Ajira Portal Login & Registaration

Ajira Portal ni mfumo mahsusi kwa ajili ya watafuta kazi wanaotaka kuomba nafasi mbalimbali ndani ya Serikalini na Utumishi wa Umma. Ajira Portal ni mfumo ambao uinasimamiwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), na inarahisisha mchakato wa kuomba kazi za serikali nchini Tanzania, ikihakikisha mchakato unaofikika kirahisi na kwa ufanisi kwa Watanzania.

Kwa watafuta kazi, kupata kazi serikalini ni muhimu sana kuwa mnatembelea ukura rasmi wa ajira portal kupitia https://portal.ajira.go.tz/. Ikiwa tayari upo registered katik mfumo huu wanaweza kuingia na kusimamia (kufuatilia muendelezo) maombi yao ya kazi, wakati watumiaji wapya wanaweza kufungua akaunti ajira portal kwa urahisi (Ukurasa rasmi wa ku-register ajira portal huonekana kama katika picha tuliyoambatanisha hapa chini). 

Jinsi ya Kuingia kwenye Ajira Portal

Ili kufurahia kikamilifu fursa za ajira serikalini, ni muhimu kuelewa jinsi mchakato wa kuingia (Login) Ajira Portal unavyofanya kazi. Hapa ni hatua za kuingia:

  1. Tembelea tovuti ya Ajira Portal kwa https://portal.ajira.go.tz
  2. Ingiza barua pepe yako au jina la mtumiaji.
  3. Weka nywila yako.
  4. Bonyeza “Login” kuingia kwenye akaunti yako.

Jinsi ya Kuunda Akaunti Mpya kwenye Ajira Portal

Kama wewe ni mtumiaji mpya, utahitaji kufungua akaunti kabla ya kuanza kuomba kazi. Mchakato wa usajili ni rahisi:

  1. Tembelea ukurasa wa Ajira Portal Login.
  2. Bonyeza kitufe cha “Register” kilicho kona ya juu ya ukurasa.
  3. Jaza fomu ya usajili kwa jina kamili, barua pepe, na nywila.
  4. Thibitisha usajili kupitia barua pepe yako.

Baada ya kusajili, utaweza kuingia na kuanza kuomba kazi.

Kumbuka: Ikiwa umesahau nywila yako, unaweza kubonyeza “Forgot your password?” ili kupata maelekezo ya jinsi ya kuirejesha.

Ajira Portal ni njia rahisi na ya haraka ya kufikia nafasi za kazi serikalini Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *